HAPA KAZI TUUUUUUUUUU
Sasa mambo yamepamba moto, hii ishu ya kutumbua majipu imefika mahala pake dahh. Juzi nilipata kazi ya kuwa mshenga. Rafiki yangu flani ambaye mambo ya fedha kwake si tatizo, ila tatizo ni namna ya kuzitumia fedha hizo kaniomba niwe mshenga wake. Alikuwa anataka kupeleka posa kwa binti mmoja ambaye ni kabila langu hivyo mimi nilitegemewa kuwa najua mila na taratibu za kutoa posa. Basi kama tulivyokuwa tumepangiwa na wakwe watarajiwa, juzi saa kumi jioni tukawasili kwa wakwe watarajiwa. Tulichelewa kama dakika tano si unajua foleni tena, hiyo ikawa nongwa ya kwanza. Wajomba wakatuambia turudi wiki inayofuata tukajifunze namna ya kuwahi, tukaanza kuomba msamaha na kubembeleza, baada ya faini ya shilingi alfu ishirini tukaruhusiwa kusikilizwa. Tulimkuta baba wa binti na wajomba wawili wanatusubiri, tukakaribishwa kwenye viti na kukaribishwa vinywaji. Tukaomba maji, unajua siku kama hii ukiomba bia kabla hawajapokea barua inaweza kuwa kisa cha kukataa kupokea barua, utasik