CHADEMA YAWA NA FURAHA BAADA YA MH.MALIWA KUTOKA RUMANDE AMBAKO AMEKAA KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA

Kile kilichokuwa kinasubiliwa kwa hamu kubwa na wananchi wa kijiji cha ruaha wilayani kilosa morogoro kimetimia baada ya mgombea wa uwenyekiti wa kijiji hicho kurudi kutoka rumande ambako amekaa ndani kwa kipindi cha mwaka mmoja. mh.maliwa ambaye ndiye alikuwa mgombea wa kiti hicho alikamatwa na wenzake wa wili na kuwekwa rumande amekaa ndani kwa kipindi cha mwaka mzima Mh. Maliwa na wenzake walikamatwa wakituhumiwa kwa makosa ya uchochezi wa kisiasa ambayo ilisababisha maandamano mara kazaa ktk kijiji hicho na hatima yake kijiji kukosa uongozi mara kazaa Mh. maliwa ndiye kipenzi cha watu kulingana na kauli na kusema kweli kwa wananchi ndiye aliyeweza kuibua uozo mwingi ambao ulikuwa ukifichwa na chama tawala ambacho kilikuwa madarakani kabla ya ofisi hiyo kufungwa na wananchi wa kijiji pamoja na maliwa kwekwa ndani kwa muda mrefu lakini bado haikuweza kupatika sababu kwa nini amekaa ndani kwa muda mrefu bila ya kufunguliwa mashtaka hatimaye maliwa na wenzake wako nje sasa HONGERA CHADEMA KWA JUHUDI

Comments