HAKIKA HUKU NDIKO KUVAMIWA KWA MAANDIKO MATAKATIFU KWENYE KUTONGOZEA WANAWAKE

Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema,
Sivema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza waYohana 4:8 "Yeye asiyependa,
hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe unamaanisha hayo
maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu
huyanena yaujazayo moyo wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na
mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31"Mbingu na nchi zitapita;
lakinimaneno yangu hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona
wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema,
Lakini wewe umewapita wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa
kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7"Mpenzi wangu, u mzuri pia pia,
Wala ndani yako hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo.
Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30"Upendeleo hudanganya, na uzuri ni
ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubaliaitakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha
baba yake na mama yake naye ataambatanana mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi
hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hikicha torati kisiondoke
kinywanimwako, bali yatafakari maneno yake mchana na
usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote
yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia
yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu
mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote
yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya
haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo
yoteyenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa
nzuri yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo
nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"

Comments